Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA 11.02 2019 SOLSKJAER KUBAKI OLD TRAFORD

Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa kudumu wa klabu ya Manchester United, lakini klabu hiyo inatazamiwa kusubiri mpaka mwisho wa msimu ili kutoa tangazo hilo. (Sun)

Kocha Rafael Benitez amempigia chapuo kiungo raia wa Paraguay Miguel Almiron, 25, tkuwa atafanya vyema klabuni hapo mara baada ya kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo. (Guardian)

Peter Schmeichel amedai kuwa mtoto wake ambaye ni kipa wa Leicester City Kasper, 32, anapanga kuihama klabu hiyo kwa kuwa hana furaha ya Maisha chini ya kocha Claude Puel. (Sun)

Wolves ndiyo vinara katika mbio za kumsajili kinda raia wa Ureno Joao Felix, 19, na tayari kocha Nuno Espirito Santo kameeleza nia ya kumtaka kiungo huyo wa Benfica. (Mirror)

Solskjaer amemuhakikishia kiungo raia wa Brazil Fred, 25, kuwa yupo kwenye mipango yake, baada ya kumng'oa kumuondoa kwenye kikosi kilichoivaa Fulham mwishoni mwa wiki. (Manchester Evening News)

Chelsea watataka kupewa mchezaji raia wa Ivory Coast iFranck Kessie, 22, endapo AC Milan watataka kumsajili moja kwa moja kwa moja kiungo wake raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24. (Daily Star)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com