Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja, MultiChoice Tanzania, Hilda Nakajumo (wa pili kulia) akielezea kwa Promosheni ya “Tia kitu, pata vituz”. Kushoto ni Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana, Meneja Rasilimali Watu, Tike Mwakitwange (wa pili kushoto), Afisa masoko na maudhui, Shumbana Walwa (kulia).
Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja, MultiChoice Tanzania, Hilda Nakajumo (wa pili kulia) akielezea kwa undani Promosheni ya “Tia kitu, pata vituz”.
Baadhi ya wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania katika picha ya pamoja wakati wa kutangaza ofa kabambe ya “Tia kitu, pata vituz”
Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia huduma zake za DStv imetangaza promosheni maalum ijulikanayo kama “Tia kitu, Pata vituz” ambapo mteja hai wa DStv atatakiwa kufanya malipo ya mwezi ya kifurushi anachotumia na kisha kupata fursa ya kuingia katika droo itakayomuwezesha kushinda kifurushi hicho hicho kwa muda wa miezi miwili zaidi bila malipo.
Akizungumza wakati wa kutangaza promosheni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja, MultiChoice Tanzania Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa Promosheni hiyo ni mahsusi kwa ajili ya wateja hai wa DStv na ni njia mojawapo ya kurudisha thamani kwa wateja wetu hawa adhimu.
"Katika promoseni hii mteja atatakiwa kufanya malipo ya kifurushi chake kabla hakijakatika, ili kupata fursa ya kuingia kwenye droo maalum itakayomuwezesha kujishindia kifurushi kile kile alicholipia kwa miezi miwili zaidi bila malipo na hivyo kuburudika na huduma zetu zikiwamo ligi mbalimbali za soka zinazotamba duniani kama EPL, La liga, Serie, sinema, tamthilia na burudani nyinginezo kedekede kwa kipindi cha miezi 3 mfululizo bila kukatika",alisema.
Naye Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana aliongeza kuwa Promosheni hiyo ya “Tia kitu, Pata vituz” ni zawadi kabambe kwa wateja wote wa DStv katika vifurushi vyote kuanzia kile cha Bomba, Family, Compact, Compact + pamoja na Premium, hususani wale walio na utaratibu wa kulipia vifurushi vyao kabla havijakatika.
Pia alieleza kuwa mteja atakayeshinda katika promosheni akihitaji kuhamia kifurushi cha juu zaidi ataruhusiwa kufanya hivyo kwa kujazia tofauti ya gharama kati ya hela (ya mwezi husika) iliyopo katika kifurushi na bei ya kifurushi anachohamia.
Alisema promosheni hii itadumu kwa kipindi cha muda wa wiki nane kuanzia Februari 19, 2019 na itaendelea hadi April 19 mwaka huu. Katika kipindi chote hicho kutakuwa na droo za kila wiki ambapo watapatikana washindi 15 kwa juma, hivyo kufanya jumla ya washindi katika kipindi cha wiki 8 kuwa 120 alieleza Mshana.
Social Plugin