Treni ya kusafirishia abiria imegongwa na basi katika mtaa wa Pipeline jijini Nairobi nchini Kenya ikitoka Embakasi.
Ajali hiyo imetokea asubuhi ya Jumanne, Februari 26 na imelihusisha basi la kampuni ya City Hoppa na hakuna aliyejeruhiwa.
Kufikia muda wa kuchapisha ripoti hii, shughuli zilikuwa zimekwama eneo hilo huku Shirika la Reli Nchini likijitahidi kutoa huduma za kuondoa basi hilo.
Hii sio mara ya kwanza kwa ajali za aina hii kutokea na katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kumeshihudiwa kadhaa. Mwaka wa 2018, treni iligongwa na lori la kusafirishia mafuta eneo la Pipeline na ajali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye Barabara ya Outering.
Social Plugin