TUME YAENDESHA WARSHA VYUO VYA ARDHI KUHUSU DHANA YA USHIRIKISHWAJI KATIKA UPANGAJI WA MATUMIZI YA ARDHI


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akitoa mada wakati wawarsha ya ushirikishwaji wa wananchi katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Bwana Kent Nillson kutoka Taasisi ya Lantmateriet nchini Sweeden akitoa mada juu ya uzoefu wa nchini kwao kuhusu upangaji wa matumizi ya ardhi.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili Ngeze Valentina wa kozi ya RDP akichangia mada wakati wa majadiliano juu ya
ushirikishwaji wa wananchi katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.
Mshiriki wa warsha Kiteri Sophia kutoka
Chuo Kikuu cha Ardhi akitoa maoni yake juu ya ushiriki wa wanawake katika hatua za upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.
Baadhi ya washiriki wa warsha wakifuatilia
kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa warsha ya upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Lantmateriet ya nchini Sweden kupitia ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweeden(SIDA) imeendesha warsha katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam na Chuo cha Ardhi mjiji Morogoro iliyohusu ushirikishwaji wa wananchi hasa makundi maalum katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.

Katika warsha iliyofanyika Chuo Kikuu Ardhi na kuhudhuriwa na Wakufunzi pamoja na Wanafunzi
wa chuo hicho, wawezeshaji walikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume Dkt. Stephen Nindi; Bw. Kent Nillson kutoka Taasisi ya Lantmateriet na Bi. Lilian Looloitai kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la CORDS ambalo hufanya kazi zake katika
Wilaya za Monduli na Longido Mkoani Arusha.

Akitoa mada katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume alielezea namna gani Sheria, na miongozo mbalimbali inayohusu upangaji wa matumzi ya ardhi inavyotambua na kuhimiza ushirikishwaji wa wananchi na kutaja makandi maalum kama vile wanawake kupewa kipaumbele katika hatua zote za upangaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi. 

Pia, Dkt. Nindi alitolea mfano wa Mwongozo Shirikishi wa Upangaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji (Participatory Land Use Management Guidelines) ambao umetamka bayana juu ya uundwaji wa kamati za upangaji na
usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi za vijiji kuwa lazima ziwe na wajumbe wanawake wasiopungua watatu.

Wakielezea uzoefu wao juu ya ushirikishwaji katika upangaji wa matumizi ya ardhi, Bw. Kent Nillson kutoka Taasisi ya Lantmateriet amesema kuwa Sweden ilianza kupangwa toka mwaka 1692 ambapo hadi hivi sasa ushiriki wa wananchi katika shughuli za upangaji na umiliki wa ardhi umeimarika kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wa mwezeshaji kutoka Asasi ya Kiraia ya CORDS, Bi. Lilian Looloitai amesema kuwa, kwa muda
mrefu sasa CORDS wamejikita katika uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Wilaya ya Monduli ambapo ushiriki wa wanawake katika zoezi hilo unaonyesha kufanikiwa. Bi. Lilian amesema kuwa kwa sasa kumekuwepo na ongezeko la idadi ya wanawake wanaoshiriki na kutoa maoni katika mikutano ya kijiji pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Warsha kama hii pia imefanyika Chuo cha Ardhi mjini Morogoro ambapo imekuwa chachu ya majadiliano
juu ya upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa njia ya ushirikishwaji pamoja na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya kusimamia sekta ya ardhi kwa kuzingatia
masilahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post