Uchawi Bariadi : BINTI AKUTWA CHINI YA UVUNGU WA KITANDA CHA BIBI YAKE HAJITAMBUI


Tukio la Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikinabushu (jina limehifadhiwa) kukutwa chini ya uvungu wa kitanda cha bibi yake, limetikisa viunga vya mji wa Bariadi, Simiyu. 



Taarifa zaidi zinaripoti kwamba, mwanafunzi huo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu tarehe 25 Januari mwaka huu hapo kijijini kwao Ikinabushu na baada ya siku tano alikutwa chumbani kwa bibi yake akiwa hajitambui.

Inaelezwa kwamba,binti huyo alikuwa akiishi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi bibi yake (Kwandu Kiuluma) na ndugu zake wengine akiwemo mama yake wa kambo na ndugu zake.

Kaka wa binti huyo, Samson Lambo amesema kuwa, aliambiwa na baba yake mdogo anayeishi Kigoma kwamba, amepokea taarifa za kupotea kwa mdogo wake na kwamba, yeye hakua akijua kuhusu ndugu mkasa huo.

Samson anasema, alipoanza kufuatilia na kuuliza, baadhi ya watu walimweleza kwamba, walikutana na mdogo wake huyo kwenye ghala maeneo ya nyumbani kwao na walipomwita alikataa na kuingia kwenye ghala hilo.

“Nilipopata taarifa hizo niliongeza wasiwasi kuhusu kupotea kwake. Kama familia tulikaa na kuamua kumtafuta kwa njia mbadala ili kujua alipo,” amesema Samson na kuongeza;

“Kwenye kikao chetu cha familia baada ya kuamini kuna mambo ya nguvu za giza, tulikubaliana kumwita mganga. Baada ya mganga kufanya dawa zake, akatuambia kuwa mtoto yupo ndani.”

Samsoni anasema, walimuuliza mganga huyo kwamba humo ndani anapatikana wapi?, ndipo walipoambiwa wakamwangalie chini ya uvungu wa kitanda cha bibi yake na kumkuta akiwa amelala hapo.

“Tulichofanya ni kumtoa kwani alikuwa na madaftari yake ya shule na alituomba maji na chakula,” amesema.

Mwanafunzi huo alisema kuwa, hana kumbukumbu yoyote kama alitoweka lakini siku moja akiwa kitandani, aliwaona watu wengi wanaume kwa wanawake wamemzunguka akiwemo bibi yake huyo.

Binti huyo amesema kuwa, alikuwa akienda shule kama kawaida na anashangaa kuambiwa kwamba hakuwa akienda shule, “mimi nashangaa kuwa eti siendi shule, najiona nilikuwa naenda shule kila siku.”

Hata hivyo, bibi huo (Kwandu) licha ya kukiri binti huyo kukutwa chini ya uvubgu wa kitanda chake, alisema hahusiki na kuongeza;

“Labda kuna watu wamefanya hivyo kupitia mimi lakini sihusiki kwa kupotea kwa mjukuu wangu.”

Deusdedit Nsimeki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ameeleza kuwa, wanamshikilia bibi huo kwa mahojiano zaidi.

Chanzo - Mwanahalisionline

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post