Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKURUGENZI PSSSF, ATEUA WENGINE WATATU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Februari, 2019 amemteua Hosea Ezekiel Kashimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund – PSSSF).

Kashimba anachukua nafasi ya Eliud Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Kashimba alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine 2 kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Augustine Emmanuel Mbokella kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya TIB (TIB Corporate Bank Limited).

Na pili, Rais Magufuli amemteua Latifa Mohammed Khamis kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara za Nje (TANTRADE).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza leo tarehe 19 Februari, 2019.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com