Katika kinachoelekea kuwa mujiza mwanamke mmoja nchini Iraqi, alifanikiwa kujifungua watoto saba kwa mpigo.
Mwanamke huyo aliyejifungua salama kupitia njia ya kawaida, anasemekana kuwa katika hali nzuri kiafya na watoto wake pia wapo katika hali nzuri.
Kulingana na ripoti ya DailyMail, mwanamke huyo aliyejifungulia katika mkoa wa Diyali ni wa kwanza kujifungua idadi hiyo ya watoto nchini humo.
Msemaji wa hospitali alimojifungulia mama huyo alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa, aliwasili katika hospitali hiyo na kujifungua watoto sita wa kike na mmoja wa kiume.
Baba wa watoto hao Youssed Fadl, alisema yeye na mke wake hawakutarajia idadi hiyo ya watoto na sasa wana watoto kumi wa kulea, wakiwamo wa mbeleni.
Pia Fadl alisema mke wake hakuwa na ufahamu angeweza kupata watoto zaidi ya mmoja kabla ya kuupata ujauzito huo.
Social Plugin