Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATU 8 WANAOTUHUMIWA KUCHOMA KITUO CHA POLISI BUNJU A WATUPWA JELA MAISHA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watu nane kutumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma moto kituo cha polisi Bunju A, jijini Dar es Salaam. Kati ya washtakiwa nane wamo wanafunzi wawili.

Jumla ya washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni 35 ambapo awali Mahakama ilikwisha waachia huru washtakiwa 17 na kubaki 18 ambapo 8 ndio wametiwa hatiani leo huku 10 wakiachiwa huru.

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa 6 ikiwemo kuchoma kituo hicho moto ambapo wanadaiwa walilitenda Julai 10, 2015.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema kitendo walichofanya washitakiwa ni unyama kwa kuchoma moto kituo hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com