Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amekemea matumizi yasiyofaa ya magari ya Jeshi la Polisi ikiwamo kubeba au kutumika kusindikiza magari yaliyopakia bangi na mirungi.
Ametoa kauli hiyo jana Ijumaa Februari 15, 2019 jijini Arusha wakati akipokea gari la Polisi lililokarabatiwa na taasisi ya Fredkin Conservation Fund kwa gharama ya Sh15 milioni.
"Mkuu wa Polisi wa wilaya sitaki kusikia hii tabia ya magari yetu kuhusika kwenye vitendo viovu, akabidhiwe dereva aliyehitimu vyema na mwenye maadili," alisema Lugola.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameishukuru taasisi hiyo kwa kuchangia shughuli za ulinzi na kuwa tayari wamejitokeza wadau watakaokarabati magari yote mabovu ya polisi wilayani humo.
Social Plugin