Mbunge wa Mkinga Tanga Dustan Kitandula
Katika kuhakikisha zoezi la uchaguzi ndani ya klabu ya Yanga linafanyika vizuri, timu hiyo imeteua kamati itakayosimamia uchaguzi huo ambao bado tarehe ya kufanyika haijatajwa.
Akionge leo kwenye makao makuu ya klabu, Kaimu Mwenyekiti na Siza Lyimo amesema mchakato wa uchaguzi unaendelea vizuri licha ya kupitia changamoto kadhaa.
''Baada ya kukutana na wenzetu wa TFF, tumekubaliana kuongeza nguvu kwenye kamati yetu na tumeongeza wajumbe ambao ni wabunge wanne na mkuu wa wilaya mmoja na kamati hiyo itaketi hivi karibuni na kupanga tarehe ya uchaguzi'', amesema Siza.
Kushoto ni Mbunge wa Igunga Seif Gulamali na Venance Mwamoto mbunge wa Kilolo
Kamati kamili ya uchaguzi
Mwenyekiti: Venance Mwamoto - Mbunge wa Kilolo
Katibu: Seif Gulamali - Mbunge wa Igunga
Wajumbe: Said Mtanda - Mkuu wa Wialya ya Nkasi
Dustan Kitandula- Mbunge wa Mkinga Tanga
Uchaguzi wa Yanga ulikuwa ufanyike Januari 13, 2019 kabla ya kuahirishwa kutokana na baadhi ya wanachama kwenda mahakamani kupinga mchakato wa uchaguzi hata hivyo walifuta kesi hiyo na kutoa mwanya kwa mchakato kuendelea.
Social Plugin