Daktari Barry Marshall ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Nobel aliyoipata kutokana na kugundua chanzo cha vidonda vya tumbo kwa kufanya majaribio katika mwili wake.
Wataalamu wengi wa Afya miaka ya nyuma waliamini kuwa bacteria hawezi kuishi ndani ya tumbo la mwanadamu kutokana na joto pia tindikali na asidi iliyopo humo. Hivyo basi iliaminika kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo unatokana na mawazo au kutokula kwa muda mrefu.
Dkt. Barry akiwa na miaka 32 aligundua kuwa vidonda vya tumbo husambazwa na bacteria anayeitwa Helicobacter pylori na alipojaribu kuwashirikisha wataalamu wengine alipingwa na hakuna aliyeamini kuwa bacteria huyo anaweza kuishi katika tumbo la binadamu kutokana na mazingira ya tindikali.
Barry Hakukata tamaa aliendelea na majaribio ili kuweza kugundua dawa ya kutibu kabisa vidonda vya tumbo na alipokwama ni jinsi ya kufanya majaribio, kwani taratibu hazikumruhusu kujaribu nadharia zake za bacteria anayepelekea vidonda vya tumbo.
Daktari huyo alifanya maamuzi magumu ya kuwameza vimelea hao wajulikanao kama Helicobacter pylori, chini ya uangalizi wa rafiki yake aitwaye Robin Warren na baada ya wiki kadhaa alikuwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Hii iliwahadaha walimwengu wa wataalamu wa afya, na alipojaribu kutumia dawa alizoziandaa mwanzo hazikufanya kazi. Akiwa mgonjwa sana hatimaye aligundua antibayotiki inayotibu vidonda vya tumbo.
Ilipofika mwaka 2007 alitunukiwa tuzo ya ya Nobel kwa ujasiri huo uliohatarisha maisha yake.
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
Social Plugin