Shirika lisilo la Kiserikali la Agape AIDS Control Program (AACP) limeendesha warsha kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kisheria ili kuandaa mkakati wa uchechemuzi wa kuishauri serikali kuifanyia marekebisho sheria ya ndoa Namba 5 ya 1971 hasa vipengele vya 13 na 17 kwa kuweka umri wa kuoa au kuolewa kuanzia miaka 18 kwa wasichana na wavulana.
Warsha hiyo ya siku tatu imeanza leo Machi 11,2019 katika ukumbi wa Virgimark Hotel Mjini Shinyanga kwa kukutanisha pamoja waandishi wa habari,viongozi wa serikali,wanasheria na wadau wa haki za watoto kutoka shirika la Agape na AIDS Foundation South Africa.
Awali akizungumza katika warsha hiyo,Meneja Miradi wa Agape, Mustapha Isabuda alisema ushawishi utakaofanywa na waandishi wa habari ili irekebishe sheria hiyo ya ndoa unalenga kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) unaolenga kupunguza ukatili kwa asilimia 50% ifikapo mwaka 2022 na.
“Sheria hii ikirekebishwa tutafikia malengo ya MTAKUWWA ya kupunguza ndoa za utotoni kutoka asilimia 37% hadi 10% ifikapo mwaka 2022 na mimba za mapema kutoka 27% hadi 5%”,alisema Isabuda.
“Hawa waandishi wa habari tusipowaambia ukweli tatizo la ndoa na mimba za utotoni halitakwisha..tunahitaji kurekebisha sheria hii ya ndoa pamoja na sera na sheria zingine kandamizi..Vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kuibadilisha jamii ndiyo maana Agape imeona vyema tuandae mafunzo haya”,alieleza.
Kwa upande wake,Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia ambaye ni Mratibu wa MTAKUWWA mkoa huo, aliwataka waandishi wa habari kuiambia ukweli jamii kuhusu wajibu wao wa kulinda watoto na kwamba ili kufanikisha MTAKUWWA ni lazima kila mtu ashiriki ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wao,Waandishi wa habari waliishauri serikali kuongeza kasi katika kurekebisha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kama vile ambavyo imekuwa ikionesha jitihada kubwa kutunga sheria zingine ikiwemo sheria ya Huduma za Habari na zile za kudhibiti Mitandao ya Kijamii.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja Miradi wa Agape, Mustapha Isabuda akizungumza wakati wa warsha kwa waandishi wa habari iliyolenga kujadilia masuala mbalimbali kuhusu namna ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja Miradi wa Agape, Mustapha Isabuda akizungumza ukumbini.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Shaban Alley ambaye ni mwandishi wa Star TV akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari Radio Faraja, Moshi Ndugulile akichangia hoja ukumbini.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Mwandishi habari wa Itv/Radio One Frank Mshana akiuliza swali wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari gazeti la Mtanzania, Sam Bahari akichangia hoja ukumbini
Lihle Mntambo kutoka Taasisi ya AIDS Foundation ya Afrika Kusini akiwasalimia waandishi wa habari kwenye warsha hiyo.
Mwanasheria ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Lightness Tarimo akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kisheria.
Wakili wa kujitegemea Maria Mwaselela akiwasilisha mada kuhusu sheria mbalimbali zinazolinda haki za watoto.
Wakili wa kujitegemea Maria Mwaselela akiendelea kuwasilisha mada.
Mdau wa haki za watoto, Lipsey Ojok kutoka Uganda akichangia hoja ukumbini.
Afisa Ustawi wa jamii halmashauri ya Shinyanga, Aisha Omari akizungumza ukumbini.
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja, Faustine Kasala (kushoto) na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Mwandishi wa habari wa Clouds Tv, Kosta Kasisi akifuatilia mada ukumbini.
Mwanasheria kutoka ofisi ya Masalu Law Attoneys, Martha Masalu akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kisheria.
Afisa Ustawi wa jamii halmashauri ya Shinyanga, Aisha Omari na Mwanasheria ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Lightness Tarimo wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari wa TBC, Greyson Kakuru (kulia) na Frank Mshana wa ITV wakiandika dondoo muhimu kwa kutumia Laptop wakati wa warsha hiyo.
Mwanasheria wa Manispaa ya Shinyanga, Patrick Muhere akitoa ufafanuzi kuhusu sheria zinazomlinda mtoto.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin