Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines imesema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote wamekufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw.
Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.
Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.
Takriban wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hakuna hata mmoja aliyeweza kunusurika na wote wamekufa, aliliambia shirika la habari la kitaifa la Ethiopia msemaji wa Ethiopian Airlines.
Social Plugin