Rais Magufuli ameonesha kukerwa na Balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia ambaye baada ya kuapishwa kuwa balozi, amekuwa akizunguka hapa nchini kwa kisingizio cha kuaga badala ya kwenda kuripoti kwenye kituo chake cha kazi alichopangiwa.
Rais ameyasema hayo leo Alhamisi March 27, 2019 wakati akimuapisha balozi mpya wa Cuba, Valentino Mlowola .
"Nakuomba Mlowola nimekuteua, uende Cuba, kuna Balozi wa Zambia nimemteua kila siku namuona anazunguka kwenye ofisi anaaga, mara kwa Waziri Mkuu, mara Makamu wa Rais, mara Zanzibar.
"Mwacheni aendelee kuaga, akimaliza kuaga, Ubalozi atakuwa hana." Amesema Rais Magufuli
==>>Zaidi, msikilize hapo chini
Social Plugin