Wakazi wa kijiji cha Kiharu kaunti ya Murang'a nchini Kenya wanaomboleza kifo cha ajuza wa miaka 76 ambaye ameripotiwa kujitoa uhai kwa kujitumbukiza kwenye choo.
Inaelezwa kuwa bibi huyo alijirusha ndani ya choo Alhamisi Machi 14,2019 baada kumuita mjukuu wake chumbani kwake na kumkabidhi simu yake ya mkono.
Familia ya Damaris Wambui Macharia iliachwa na mshangao mkubwa huku ikiwaza nini kilichomfanya ajuza huyo kutekeleza kitendo cha aina hiyo.
Marehemu hakuwa ameonyesha dalili zozote kwamba angejitoa uhai.
Kulingana na mmoja wa jamaa wake, Damaris alikuwa akmpigia mjukuu wake simu kila mara akitaka aende chumbani mwake ila hakuwa akimwelezea alichotaka.
Mumewe marehemu Moses Macharia alisema alipokea kifo cha Damaris kutoka kwa mjukuu wake aliyempigia simu akiwa kwenye hoteli yake iliyoko katika barabara ya Murang'a kuelekea Migoiri.
Macharia alisema mkewe amekuwa akilalama hapo awali kuhusu maumivu tumboni ila alikuwa amepata nafuu na alikuwa ashaanza kufanya kazi za nyumbani.
Kisa hicho kiliwashangaza wengi kwani marehemu hakuwa ameonyesha dalili zozote za kujitoa uhai.
Chanzo- Tuko
Social Plugin