Basi la Kampuni ya BM Coach limepata ajali ya kupinduka jana Jumatatu, Machi 4, 2019 majira ya alasiri wakati likijaribu kukwepa Kichwa cha Treni (Kiberenge) maeneo ya Chekelei wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kuwa dereva wa Basi la BM Coach, akitoka Arusha kuelekea Morogogo alishindwa kusimama katika kivuko cha Treni eneo la Chekelei Mombo, barabara kuu ya Segera/Same.
Ameongeza kuwa, wakati kichwa cha Treni kikikaribia eneo hilo na ndipo basi hilo likagongwa na kulala ubavu huku kichwa hicho cha Garimoshi kikiendelea na safari bila kusimama.
Hakuna taarifa ya vifo kwa sasa isipokuwa abiria kadhaa wamejeruhiwa akiwemo dereva wa BM Coach ambaye ameumia sana.
Social Plugin