Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAOMBI YA JOSHUA NASSARI KUPINGA KUVULIWA UBUNGE


Mahakama Kuu kanda ya Dodoma imetupilia mbali maombi ya Joshua Nassari ya kupinga kitendo cha Spika wa Bunge kumvua ubunge wa Arumeru Mashariki kutokana na utoro bungeni

Akisoma maamuzi hayo leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji wa Mahakama Kuu Dodoma, Latifa Mansour ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.

Kifungu kingine kilichombana Nassari ni cha kanuni ya 146 (2) kwamba alijifukuzisha mwenyewe kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge bila taarifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com