Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema uamuzi uliofanywa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo umeonyesha na kuthibitisha kwamba utawala uliopo unaozingatia misingi ya Katiba ambayo CCM imeutekeleza.
CCM ilitoa kauli hiyo jana Jumatatu Machi 18, 2019 kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole baada ya Maalim Seif kutangaza kuhamia ACT- Wazalendo baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa hukumu yake kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF.
“Huu ni Utawala wa sheria unaoruhusu mihimili ya dola kufanya kazi pasina kuingiliwa, watu wanazo haki kufanya uamuzi wa kisiasa kwa kujiunga na chama chochote.
“Hili ni fundisho kwa wale ambao wanasema mtu kujiunga na chama kingine maanake kanunuliwa, hii imedhihirisha ni uhuru wao wa kisiasa,” alisema Polepole
Social Plugin