Hatimae Chama cha wananchi CUF leo Jumanne Machi 26,2019 kimefanikiwa kudhibiti Makao makuu ya chama hicho yaliopo Mtendeni mjini Unguja na kupachika bendera zoezi ambalo lilisimamiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi.
Zoezi hilo limeongozwa na mjumbe wa bodi ya wadhamini, Mussa Haji Kombo pamoja na wanachama wengine wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kombo amesema wamelazimika kuweka bendera wakifahamu kuwa ofisi hiyo ni miongoni mwa mali za chama hicho.
Social Plugin