Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupitia kwa Jaji Dk Benhajj Masoud Leo Machi 18,2019 imetoa hukumu na kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi (CUF) baada ya kushinda kesi kutokana na mvutano wa uongozi.
Jaji Masoud amesema kuwa msajili wa vyama vya siasa ana mamlaka ya kutoa msimamo na ushauri alioutoa kuhusu uhalali wa Profesa Lipumba.
Amesema mamlaka ya msajili hayaishii tu katika kusajili vyama na kupokea mabadiliko ya viongozi na kwamba vinginevyo asingekuwa na mamlaka ya kuvifuta vyama.
Social Plugin