Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HALMASHAURI 31 ZATAKIWA KUJIELEZA KWA WAZIRI KWA KUTOKUTENGA FEDHA ZA LISHE

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa, Seleman Jafo, ameagiza ndani ya siku kumi na nne kwa Halmashauri therathini na moja, ambazo zilishindwa kuwasilisha fedha zilizotengwa kwa ajiri ya lishe katika halmashauri zao kujieleza kwanini hazikufanya hivyo.

Waziri Jafo  ameagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua kikao kilichowakutanisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, waganga wakuuwa mikoa, wawakilishi toka taasisi ya chakula na wadau wa maendeleo,waliokutana kutathmini hali ya lishe hapa Nchini na mahali walipofikia katika mpango wa kwanza wa lishe wa august 2018 hapa Nchini.

Waziri Jafo amesema kuna halmashauri therathini na moja hazikutoa fedha zilizotengwa kwa ajiri ya kutekeleza hali ya lishe katika maeneo hayo hali iliyosababisha kushindwa kutekelezwa kwa malengo ya lishe ndani ya halmashauri hizo.

“Ni agize ndani ya siku kumi na nne halmashauri ishirini na moja zitoe maelezo ya kina kwa wakuu wao wa mikoa kwanini hazikutoa fedha zilizotengwa ndani ya halmashauri hizo kwa ajiri ya lishe kwanini hazikufika”

“Na ninyi wakuu wa mikoa baada ya siku hizo kumi na nne baada ya hapo nipate maelezo ya kwanini zilishindwa kutekeleza mikataba hiyo wakati halmashauri nyingine zaidi ya mia mija zimetekeleza” alisema Jafo

Kwa upande mwingine Waziri Jafo amekemea vikali tabia ya wakuu wa idara ambao hawafiki kwenye semina zinazohusu lishe na kuwaagiza watumishi wengine ambao hawana uelewa katika sekta hizo na kusababisha elimu hiyo kutokufikia mahala husika kwa uzembe wa wakuu wa idara hizo.

“Kuna tabia ya wakuu wa idara kushindwa kuhudhuria semina, hawahudhurii au wana waagiza watumishi wengine ambao hawana uelewa juu wa mambo ya lishe na  hii inasababisha kuwa na gepu kubwa la maamuzi  na ninaomba wakuu wa mikoa muwe wakali kwenye mambo kama haya” alisema.

Waziri Jafo pia ameagiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya lishe kwa akina mama wajawazito wanapofika kliniki kabla ya kujifungua na watengeneze vipeperushi ambavyo  vitasaidia kupeleka elimu kwa jamii na kuchukua hatua.

Nae muwakilishi wa wakuu wa wilaya Daniel Chongolo, ambae ni mkuu wa wilaya ya kinondoni, amewaomba wadau wa maenendeleo kupelekwa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa wa lishe ili kujenga kizazi imara cha baadaye.

Alisema endapo tusipokabiliana na changamoto hii kuna wakati tutakuta kuna sehemu kuna kizazi ambacho hakina uelewa kabisa kwenye maswala ya kielimu kwa sababu ya kutopata lishe bora.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka shilika  la GAIN linalijihusisha na elimu ya lishe, Archard Ngamela  amesema, changamoto kubwa kwenye lishe ni wasindikaji wadogowadogo hawaweki virutubisho katika bidhaa za vyakula na kusababisha kuenea kwa tatizo la lishe.

“Changamoto kubwa tunayokutana nayo ni  tabia ya hawa wajasiliamali wadogo au hawa wasindikaji wa viwanda vidogovidogo hawaweki virutubisho kwenye bidhaa zao na hii ni changamotokatika lishe hapa nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com