Baadhi ya hisia tunazohisi kuwa ni za binadamu si sisi pekee tunaokuwa nazo
Uwezo wa kuwa na raha, maumivu na hofu si binadamu pekee wamaokuwa nao. Ukweli ni kwamba uwezo huu wanao wanyama wa jamii mbali mbali.
Lakini ni vipi kuhusu hisia mbaya kama vile kuomboleza kifo cha mpendwa au kuhisi hasira wakati unapokosa kutendewa haki ?
Mapinduzi ya kibaiolojia na tabia pamoja na sayansi ya ubongo yamebaini kuwa mifumo yetu ya neva inafanana sana na ile ya baadhi ya wanyama, hasa wale wa jamii ya mamalia.
Sawia na hayo, baadhi ya hisia ambazo mara nyingi tunafikiri ni za binadamu si zetu peke yetu.
Ifuatayo ni mifano mitano iliyochukuliwa kutoka kwneye kitabu "The Emotional Intelligence of Animals", kilichoandikwa na mtaalamu wa tabia za wanyama Muhispania Pablo Herreros.
1. Hisia ya kutendewa hakiusipomtendea haki nyani aina ya capuchin tegemea kukabiliana na hasira yake
Watu wengi wanaweza kutofautisha kati ya wanapotendewa haki na pale ambapo hawajatendewa haki. Nyani aina ya capuchin pia ana utambuzi huu.
Katika utafiti uliofanyw ana kituo cha Yerkes cha Atlanta, wanayama hawa waligoma kuonyesha ushirikiano na watafiti walipohisi kuwa hawakutendewa haki.
Watafiti walilipatia kundi la nyani aina ya capuchin vipande vya matango badala ya vipande vya plastiki.
lakini wakampatia nyani mmoja wao zabibu- chakula wanachokipenda sana.
baada ya kufanya hivyo mara, waliosalia wakagoma kuendelea kufanyiwa uchunguzi. baadhi yao hata waliwarushia vipande vya matango biandamu.
2. Nia ya kulipiza kisasiNdovu wamekuwa wakifahamika kwa ulipizaji kisasi dhidi ya watu
Karibu sote binadamu wakati mmoja tumekuwa na hisia ya kulipiza kisasi wakati mmoja. Ni kwa nini binadamu wasiwe na hisia sawa na sisi?
Mwaka 2016 kundi la tembo waliuvamia mji wa Ranchi, uliopo mashariki mwa India, na kuwalazimisha wakazi kutoroka makazi yao ili kuokoa maisha yao. Wanyama hao walikuwa wakiusaka mwili wa ndovu jike aliyekuwa amekufa baada ya kuanguka kwenye mfereji wa maji ya umwagiliaji wa mashamba.
Wanyama wnaweza kuonyesha hasira na ulipizaji wa kisasi dhidi ya watu wanaowatunza.
Na sokwe hukumbuka ni nani ni marafiki na ni nani ni maadui zao. Wakati adui anapomshambulia rafiki, wanaweza kulipiza kisasi.
3. Upendo wa mamaUpendo wa sokwe ambaye ni mama kwa mwanae unaweza kuwa ni thabiti
Binadamu huwa wanakuwa na upendo na kuwajali vizazi vyao. Lakini pia wanyama wengine wana uwezo wa kuonyesha upendo sawa na huo wa mzazi kwa mwanae.
Christina,sokwe kutoka Tanzania, alionyesha upendo hata kwa mwanae ambaye alizaliwa na ugonjwa wa Down syndromena ngiri uliomzuwia kukaa chini.
Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Tokyo walishuhudia namna wakati mwingine mama anavyoweza kuacha kula ili kumjali mwanae.
hakutaka yeyote ambebe mwanae wa kike, kana kwamba alifahamu kuwa hakuna anayeweza kumjali mwanae kuliko yeye. Mtoto huyo wa kike alikufa akiwa na umri wa miaka miwili.
Pablo Herreros pia aliandika kuhusu mama wa ndovu aambaye alitenganishwa na mwanae ambaye alifunzwa na kuwaburudisha watalii nchini Thailand.
Miaka mitatu baadae, baada ya juhudi za wahifadhi wa wanyamapori kumtafuta mwana wa tembo huyo, waliungana tena katika makazi ya tembo . Mama na mwanae walisimama wima kwa saa nzima . Wakaanza kugusanisha pe,mbe zao huku kila mmoja akimtomasa mwenzake.
4. Kuvunjika moyoNdege aina ya Macaw wanaweza kufa kwa kuvunjika moyo
Kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi huwafanya watu waumie sana.
Ndege aina ya Macaw ambao ni waaminifu sana kwa wapenzi wao katika kipindi chote cha maisha yao, huwa wanaumia sana wanapowapoteza wapenzi wao.
Pale mmoja kati ya wapenzi anapokufa ghafla , mwingine huwa anapata ugumu wa kuishi peke yake: mara nyingi huwa aliyebaki anashindwa kula na kuwa dhaifu sana.
baadhi huwa dhaifu kiasi cha nkushindwa kuishi kwenye viota vyao na kuanguka chini kwenye miamba. Ni kama aina fulani ya kifo cha mapenzi ?
5. Huruma na farajaPanya buku wanauwezo wa kufarijiana
Binadamu wanauwezo wa kuwafariji binadamu wenzao na kuhisi kuwahurumia.
Mwaka 2016 utafiti uliochapishwa kwenye jarida la kisayansi ulibaini kuwa panya hawa huwa wanawafariji wenzao wanaohisi msongo wa jambo fulani , jambo ambalo watafiti wanalielezea kama ushahidi wa huruma.
Katika vipimo vya uchunguzi, panya wawili walitenganishwa. mmoja wao alipigwa na umeme kidogo.
Walipokutanishwa tena, panya ambaye hakupigwa na umeme alijaribu kumfariji mwenzake kwa kumlamba kwa muda mrefu kuliko wanyama wenginekatika kikundi ambao walikuwa pia wametenganishwa na ambao hawakupigwa na nguvu ya umeme.
Kwa mujibu wanasayansi hii inaonyesha faraja kwa inayosaidia kuondoa msongo kwenye ubongo jambo linalosaidia kuachiliwa kwa homoni za ubongo zinazofahamika kama "homoni za upendo " - ambazo huboresha maisha yao.
Tafiti nyingine zimebaini kuwa sokwe, ndovu na mbwa huwafariji waathiriwa wenzao wa mashambulio.
Chanzo- BBC
Social Plugin