Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TFF WAIKANA JEZI YA MSALABA


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetolea ufafanuzi juu ya uwepo wa msalaba kwenye jezi ya timu ya taifa 'Taifa Stars', ambayo imezua gumzo mitandaoni, na kusema kwamba hawaitambui jezi hiyo.

Kwenye taarifa iliytolewa na Afisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo kwa vyombo vya Habari, imesema kwamba wao hawahusiki na jezi hiyo, na kutoa onyo kali kwa watakaokutwa wanaiuza au kuisambaza.

“TFF haihusiki na jezi hiyo ambayo si sehemu ya jezi inayotumiwa na Timu ya Taifa, tunawaonya wote wanaoza jezi ambazo si sahihi, kuacha mara moja kabla TFF haijachukua hatua kali”, imeeleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni kumezagaa jezi ambazo zinasadikiwa kuwa za Taifa Stars zenye picha ya msalaba kifuani, na kuleta gumzo mitandaoni huku kukiibuliwa masuala ya tofauti ya imani za kidini.

Isome taarifa yote hapa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com