JINSI KAZI ZINAVYOUA WATU NA HAWAJALI

Jeffrey Pfeffer anaposema kuwa ''kazi zinawaua watu na hakuna anayejali,'' hasemi kwa njia ya mafumbo.

Anasema kwa hakika kabisa kutokana na utafiti alioufanya kwa miongo kadhaa, nchini Marekani na duniani kwa ujumla.

Profesa Pfeffer kutoka shule ya biashara ya Chuo cha Stanford na mwandishi na mwandishi msaidizi wa vitabu 15 kuhusu muundo wa kampuni na masuala ya uongozaji rasilimali watu, ametoa hoja katika kitabu chake cha hivi karibuni kiitwacho , ''Kufa kwa ajili ya Mshahara'' Jinsi mifumo ya kazi inavyoathiri na hata kusababisha kukatisha maisha ya watu.

Katika kitabu hicho anazungumzia tuko la Kenji Hamada, mwenye miaka 42 aliyekufa kwa mshtuko wa moyo akiwa kwenye dawati lake kazini jijini Tokyo.Nilifanya kazi saa 72 kwa wiki na ilikua inanichukua saa mbili kufika kazini.

Kabla ya kifo chake, alifanya kazi siku 40 mfululizo bila kupumzika na mjane wake anasema Kenji alikuwa na msongo mkubwa

Huu ni moja kati ya mifano iliyokuwa kwenye chapisho lake, ambapo mwandishi anaeleza madhara ya mfumo wa kazi ambao wakati mwingine ''si ya kibinaadamu'' kutokana na majukumu makubwa ya kazi.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowekwa na Pfeffer,nchini Marekani, asilimia 61 ya wafanyakazi wanaona kuwa msongo umewafanya waumwe na asilimia 7 wanasema walilazwa kutokana na sababu zinazohusiana na kazi.

Makadirio yake ni kwamba msongo una uhusiano na vifo vya wafanyakazi 120,000 wa Marekani.Wafanyakazi hupoteza maisha kutokana na majukumu mengi ya kazi

Kwa mtazamo wa kiuchumi, msongo umewagharimu waajiri zaidi ya dola za Marekani 300,000 kwa mwaka nchini Marekani.

Katika kitabu chako umeeleza kuwa kuna mfumo wa ufanyaji kazi unaowaua watu.Ni ushahidi gani ulionao kuhusu hili na ni kwa jinsi gani mfumo wa kisasa wa ufanyaji kazi unawaathiri waajiriwa?

Kuna ushahidi wa madhara ya kiafya.Saa nyingi za kufanya kazi,kupunguzwa kazi, kukosa bima ya afya, masuala ya kiuchumi, migogoro kwenye familia na maradhi.

Kazi sasa imekua si ya kibinaadamu.Kwa upande mwingine, makampuni yameacha kuwajibika kwa ajili ya wafanyakazi wao.

Lakini changamoto za kiuchumi zimeongezeka, hofu ya kukosa ajira pia inaongezeka.

Katika Benki za uwekezaji, kwa mfano, kuna namna ya ufanyaji kazi, unakwenda nyumbani kwako kuoga na kurejea ofisini.

Katika mfumo huo, waajiriwa wengi huingia katika uraibu wa madawa, kwa sababu wanaishia kutumia Cocaine na madawa mengine ili wawe macho.

Mfanyakazi wa kiwanda, rubani wa ndege, mwendesha lori, wana idadi ya saa za kufanya kazi.

Lakini kuna kazi nyingine hakuna saa maalumu za kazi.

Nchini Marekani, sababu ya tano ya vifo ni sehemu ya kazi.

Lakini nani anawajibika kwa vifo hivi?

Waajiri na serikali zinawajibika kwa kutochukua hatua yoyote kuhusu suala hili.

Ni kazi kubwa tunapaswa kufanya kitu kwa ajili ya kukomesha hili.Lakini hatutaweza kufanya chochote kama mtu mmojammoja.

Kama unataka kutatua tatizo yapaswa kuwa katika utaratibu ambao utatoka kwa mtindo wa sheria.

Mazingira mabaya ya kazi husababisha maradhi kama vile sukari na shinikizo la damu.

Lakini tukizungumzia gharama,makampuni yanaweza kuleta hoja kuwa kufanya mabadiliko katika mfumo wa kazi kutaathiri kipato cha kampuni.

Hii si kweli, anasema Profesa Pfeffer.''Tunajua kuwa watu walio katika msongo wa mawazo wako katika nafasi kubwa ya kuacha kazi''.Tunajua kuwa wafanyakazi wasio sawa kisaikolojia hawawezi kuizalishia kampuni inavyopaswa''.

Alitolea mfano kuwa inafahamika kuwa Marekani na Uingereza zaidi ya 50% ya siku za kazi hupotea kwa sababu ya wafanyakazi kutokuwepo kutokana na msongo wa kazi.

Hivyo kuna athari kubwa kwa mfanyakazi mgonjwa anayekwenda kazini na asifanye kazi kama anavyotakiwa.Hali hii huigharimu kampuni.Wafanyakazi wanapaswa kuzijali afya zao

Wafanyakazi wanapaswa kujijali

Kwa upande wa wafanyakazi, Profesa ameandika kuwa watu wajijali.Lakini ameulizwa swali kuwa itakuwaje ikiwa muajiriwa akadai kuboreshewa mazingira ya kazi na kuna uwezekano akaishia kufukuzwa?

Je mazingira ya kazi yatabadilishwaje?

Profesa anasema, kwanza waajiriwa wanapaswa kujali afya zao.

Ikiwa unakwenda kazini, mahali ambapo huwezi kuoanisha maisha ya kazi yako na familia, unapaswa kuacha kazi hiyo.

Jambo jingine ni kwamba watu wanapaswa kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post