Mbunge wa Bunda mjini, Esther Bulaya amesababisha kuahirishwa kwa kesi inayomkabili yeye pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe kutokana na kutofika mahakamani.
Leo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikuwa ikisubiri mashahidi wa Upande wa Jamhuri kwa ajili ya kesi hiyo Na. 112/2018.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi 16/4/2019 kutokana na kwamba Mbunge huyo ni mgonjwa hivyo kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo.
“Mheshiwa hakimu, Bulaya ni mgonjwa amefanyiwa upasuaji Machi 23, 2019 katika Hospitali ya Aga Khan na kuruhusiwa kutoka hospitali hapo Machi 26, 2019, hivyo kutokana na hali yake ameshindwa kufika mahakamani hapa kusikiliza shauri hili,” amedai mdhamini wa Bulaya, Ndeshukurwa Tungaraza
Bulaya na Viongozi wengine saba wa wa CHADEMA wanatuhumiwa kwa kosa kufanya maandamano haramu yaliyopelekea kifo cha mwanafunzi wa Akwilina, mwanzoni mwa mwaka uliopita.
Social Plugin