Kila mfanyakazi katika viunga vya ofisi za Clouds Media Group anaonekana kukumbwa na fadhaa. Ni ngumu kuamini kuwa ndani ya siku 10 wamepokea taarifa za msiba wa watu wawili muhimu kwao.
Mtangazaji Ephraim Kibonde amefariki siku nane baada ya Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa kampuni hiyo, Ruge Mutahaba kufariki Februari 26, 2019.
Katika ofisi za Clouds Media group, wafanyakazi wameonekana wamekaa kimafungu sehemu ya kuegesha magari kila mmoja akiwa na simanzi na wengine wakilia.
Social Plugin