Aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds Media Group (CMG), Ephraim Kibonde amezikwa leo Machi 9,2019 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam majira ya saa kumi jioni.
Amezikwa na maelfu ya watu ambao ni ndugu, jamaa na marafiki aliokuwa akifanya nao shughuli mbalimbali enzi za uhai wake na wengine waliomjua kupitia kazi yake ya utangazaji.
Kibonde amefariki dunia Machi 7 mwaka huu baada ya kuugua Presha kwa muda mfupi katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza.
Ameacha watoto watatu, wa kike wawili na mmoja wakiume.
Waziri wa habari, utamaduni na michezo, Harrison Mwakyembe akiweka shada la maua kwenye kaburi la Kibonde.
Wabunge akiwemo Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, Zitto Zuber Kabwe na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haul ‘Prof. Jay’ wakiwa wakiweka shada la maua kama ishara ya kumuaga mpendwa wao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiweka shada la maua.
Social Plugin