Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemkabidhi maalim Seif Hamad kadi namba moja ya ACT Wazalendo ambayo imeshalipiwa kwa kipindi cha miaka 10.
"Mimi nina kadi namba nane.. Kadi namba moja kuna mtu aliiwahi na kwa heshima kadi hii imekwenda kwa Maalim Seif",amesema Zitto.
Shughuli ya kukabidhi kadi hizo inaendelea kufanyika leo Machi 19, 2019, makao makuu ya ACT- Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo,
Katika makabidhiano hayo, Zitto amesema hiyo namba kumi ambayo amekabidhiwa Duni ni kama mchezaji wa timu ya Liverpool.
''Kadi maalumu zimekuwa nyingi kweli kweli maana tumepokea watu muhimu mpaka ilibidi tunyang'anyane lakini namba 1, 6, 10 na 17 zote zimekwenda kwa viongozi walioambatana na Maalim'.
''Naomba tusiingie kwenye mtego wa msajili, hivyo tutakwenda kusajili kadi zetu kwenye matawi yetu ili tusije kuulizwa kama makao makuu kuna tawi'' ,amesema Zitto Kabwe.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Maalim Seif amesema yeye ni mara ya kwanza kukanyaga ofisi za ACT- Wazalendo lakini anajiona ni mwenyeji.
Social Plugin