Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : MADIWANI WA MIKOA MITANO WAFANYA ZIARA AGAPE NA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA VYA TGNP MTANDAO KISHAPU

Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao kutoka Mikoa ya Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga na Kigoma wametembelea Shirika la Agape AIDS Control Programme na vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga. 

Lengo la ziara hiyo ya siku mbili iliyoanza Machi 27 na kumalizika Machi 28,2019 ni kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vituo vya Taarifa na Maarifa wilayani Kishapu na Washirika wake likiwemo Shirika la Agape. 

Mwezeshaji wa ziara hiyo,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao alisema katika siku ya kwanza ya ziara,walitembelea kituo cha Taarifa na Maarifa cha kata ya Ukenyenge,kukagua vyumba vya usiri kwa wanafunzi wa kike na vyoo katika shule za msingi Kanawa na Bulimba,zahanati ya Negezi na Gender Club katika shule ya sekondari Ukenyenge. 

“Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa hiyo mitano walijifunza namna vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya ya Kishapu jinsi vinavyoshirikiana na jamii na viongozi wa serikali kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii”,alieleza Amani ambaye pia ni Meneja Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi unaotekelezwa na Agape wilayani Kishapu. 

“Washiriki wa ziara hii pia wametembelea shirika la Agape lenye makao yake Makuu katika Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga linalojihusisha na masuala ya ulinzi wa mtoto,utoaji msaada wa kisheria,kutokomeza mimba na ndoa za utotoni,ukatili wa kijinsia,malezi na makuzi bora ya mtoto”,aliongeza Amani. 

Aidha alisema wakiwa katika shirika la Agape,Washiriki wa ziara hiyo pia waliwatembelea wanafunzi wahanga wa mimba na ndoa za utotoni wanaosoma katika shule ya Agape Knowledge Open School inayomilikiwa na Agape iliyopo katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga. 

Miongoni wa madiwani hao akiwemo Pessa Pessa kutoka kata ya Bwakira Chini halmashauri ya wilaya ya Morogoro waliishukuru TGNP Mtandao kwa kuwazesha kufika mkoani Shinyanga kujionea mambo mazuri yanayofanywa na Vituo vya Taarifa na Maarifa na shirika la Agape katika kupiga vita matukio ya ukatili wa kijinsia. 

“Kwa kweli bila TGNP Mtandao tusingeweza kuyafahamu mambo mema yanayofanywa na wenzetu katika kuhakikisha watoto wanalindwa lakini pia kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia”,aliongeza Festo Mwalyego ambaye ni diwani wa kata ya Tembela halmashauri ya wilaya ya Mbeya. 

Naye Stimar Heda John (kata ya Ijombe halmashauri ya wilaya ya Mbeya),aliwaomba viongozi wa serikali kutembelea shirika la Agape kwani linafanya kazi kubwa kuwasaidia watoto wanaokumbana na vitendo vya ukatili hivyo serikali ione namna ya kuwaongezea nguvu ili kusaidia Watanzania wengi zaidi. 

ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na TGNP Mtandao kutoka Mikoa ya Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga (Kishapu) na Kigoma wakiwasili katika Ofisi za Shirika la Agape AIDS Control Programme katika kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga leo Machi 28,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agape,Lucy Maganga akiwakaribisha Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa Morogoro,Mbeya,Mara,Shinyanga (Kishapu) na Kigoma. 
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Agape,Lucy Maganga akikaribisha madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa.
Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika la Agape katika kulinda watoto na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea historia ya Shirika la Agape.
Diwani wa Viti Maalum kata ya Ukenyenge wilaya ya Kishapu,Josephina Malima akizungumza wakati wa ziara hiyo na kueleza namna wanavyoshirikiana na vituo vya taarifa na maarifa,serikali na wadau mbalimbali likiwemo shirika la Agape na TGNP Mtandao katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Diwani wa kata ya Tembela halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Festo Mwalyego akielezea jinsi Imani za kishirikina zinavyochangia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake katika jamii na kuitaka jamii kuepukana na imani hizo. 
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Fredina Said akielezea shughuli wanazofanya wilayani Kishapu kupiga vita ukatili wa kijinsia. 
Diwani wa Kata ya Ijombe halmashauri ya wilaya ya Mbeya,Stimar Heda John akipongeza kazi zinazofanywa na shirika la Agape katika kulinda haki za watoto.
Meneja Fedha wa Shirika la Agape Nkwimba Ng'homano Lugisi (wa pili kushoto) akieleza namna wanavyowahifadhi kwa muda mabinti waliofanyiwa vitendo vya ukatili katika chumba maalum kilichopo katika ofisi za shirika la Agape.
Nje ya chumba cha kuhifadhi mabinti waliofanyiwa vitendo vya ukatili . Kushoto ni Mwezeshaji wa ziara ya Madiwani na Wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ,Peter Amani kwa niaba ya TGNP Mtandao akielezea jambo kwa Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa.
Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa wakiondoka katika ofisi za shirika la Agape.
Hapa ni katika shule ya Agape Knowledge Open School ambapo mabinti wahanga wa mimba na ndoa za utotoni wanapewa elimu ya kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.Kulia ni Peter Amani akitambulisha Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga waliotembelea shule hiyo.
Peter Amani akielezea namna mabinti wanavyosoma katika shule hiyo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo,Kalunga Zacharia akielezea changamoto zilizopo katika shule hiyo kuwa ni uhaba wa madarasa,mabweni,vitabu na madawati.
Diwani wa kata ya Bwakira Chini halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Pessa Pessa akilishukuru na kulipongeza shirika la Agape kuwapatia elimu watoto hao ambao ni wahanga wa mimba na ndoa za utotoni na kuahidi kushirikiana nao katika kuendelea kuwapatia msaada zaidi ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Songwa wilayani Kishapu Rahel Madundo akiwasisitiza watoto hao kusoma kwa bidii.
Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga wakiongozwa na wanafunzi kutembelea shule hiyo.
Madiwani na wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka mikoa ya Mbeya,Morogoro,Kigoma,Mara na Shinyanga,viongozi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya Madiwani na viongozi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.
Wawakilishi wa vituo vya taarifa na maarifa na viongozi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malundev- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com