Jamaa mmoja mwenye umri wa makamo ameripotiwa kufariki dunia baada ya kugongwa na basi lililokuwa likiendeshwa kwa kasi kutoka mjini Kisumu kuelekea Nairobi nchini Kenya.
Tukio hilo limetokea Alhamisi Februari 28,2019 eneo la Kachok katika barabara kuu ya Kisumu kuelekea Nairobi.
Inasemekana jamaa huyo alifanya kitendo hicho saa chache tu baada ya kugombana na mpenziwe ambapo inasemekana kumfumania mpenziwe akifanya mapenzi na rafiki wake wa karibu.
Aliyeshuhudia ajali hiyo alisema marehemu alijirusha katikati ya barabara kutoka kwenye daraja lililo karibu na shule ya upili Lions na kukanyagwa vibaya na basi lililokuwa likiendesha kwa kasi.
Inasemekana marehemu alikuwa amegombana na mpenzi wake saa chache kabla ya kutekeleza kitendo hicho.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga.
Kisa hiki kinatokea siku chache tu baada ya kingine sawa kuripotiwa mjini Naivasha eneo la Kayole ambapo jamaa mmoja pia alijirusha barabarani na kugongwa na gari lililomuua papo hapo.
Social Plugin