Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AJIUA KWA KUJIRUSHA BONDENI BAADA YA KUUA MWANAE KISA MGOGORO NA MKEWE

 Hali ya majonzi imegubika kaunti ya Kitui nchini Kenya baada ya jamaa kumuua mwanawe mwenye umri wa miaka sita kisha kujirusha kwenye bonde akavujika shingo na miguu na kufariki dunia.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 27 alimkata mwanawe shingo Jumamosi, Machi 16,2019 kisa kilichowaghadhabisha wenyeji pakubwa.

 Akithibitisha kisa hicho Jumapili, Machi 17,2019 Kamishna wa kaunti hiyo Jacob Ouma ameeleza kuwa jamaa huyo aliyekuwa na tofauti za kinyumbani na mkewe alisafiri kutoka Mombasa walikoishi pamoja.

Alisafiri hadi Kitui kumuua mwanawe kufuatia mzozo na mkewe mjini Mombasa. 

''Alifanya unyama huo usiku wa jana kabla kuenda mafichoni lakini akapatwa na wenyeji wenye hasira waliomsaka na kumpata katika kijiji cha Kamukenga Hills leo hii,’’ Kamishna wa kaunti hiyo Jacob Ouma alieleza.

Kulingana na ripoti, jamaa huyo aliweza kuwaponyoka jamaa hao kabla kujirusha kwenye bonde. 

"Alijirusha bondeni na kuvunjika shingo na miguu. Kutokana na urefu wa bonde hilo, hangeweza kunusurika,'' aliongezea. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti alikopelekwa mwanawe awali. 

 Mkewe marehemu alipoteza fahamu baada yakupata habari hizo na kulazwa katika hospitali kuu wa Coast anakoendelea kupata ahueni. 
Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com