Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tazama Picha :MAZISHI YA RUGE MUTAHABA...AZIKWA KISHUJAA KIJIJINI KWAO


Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba umezikwa kishujaa nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru Kata ya Karabagaine Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera huku mamia ya watu wakiwemo viongozi wa serikali wakishiriki mazishi hayo.


Zoezi la kuzika mwili wa Ruge lilianza kwa Ibada ya mazishi ambayo iliongonzwa na Katibu wa Parokia ya Itahwa, Anatory Kyatwa huku nyimbo za kihaya zikipamba tukio la mazishi.
Mtoto wa marehemu Ruge akiwa mashada katika kaburi la marehemu baba yake ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, akiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.
Wazazi, familia, wakiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.
RC Makonda akiweka shada katika Kaburi la Ruge.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba akiweka shada.
Awali wakati wa tukio la kuaga mwili wake katika viwanja vya Gymkhana, Maaskofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba walimtaja Ruge kama kijana jasiri mzalendo na mfano wa kuigwa.

Mama wa marehemu Ruge Mutahaba (wa pili kushoto), akifuatiwa na mumewe wakiwa na aliyekuwa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala, dakika chache kabla ya mwili wa mtoto wao marehemu Ruge Mutahaba Kuingizwa kaburini, kijijini Kiziru. Rip Ruge






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com