Kamati Kuu ya chama kikuu cha upinzani nchini (Chadema) leo inakutana ili kupokea taarifa na kujadili mwenendo wa hali ya siasa nchini.
Taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho imeeleza kuwa, kikao hicho ni cha siku moja na kilichofanywa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema toleo la mwaka 2016.
Kikao hicho kitaongozwa na Mbowe, ikiwa ni baada ya kukosa vikao kadhaa kutokana na kuwekwa rumande katika Gereza la Segerea tangu Novemba mwaka jana mpaka alipopata dhamana tarehe 7 Machi 2019.
Kazi zinazotarajiwa kufanywa na kamati hiyo ni pamoja na kupokea taarifa na kujadili mwenendo wa kisiasa nchini, na kisha kuchukua mwelekeo baada ya mjadala wa taarifa hiyo.