Balaa limezidi kumuandama Mchungaji wa kanisa la Alelluia Ministry la Afrika Kusini, Alph Lukau, baada ya baadhi ya wanawake kujitokeza na kuelezea jinsi walivyodhalilishwa kingono na mchungaji huyo.
Miongoni mwa walalamikaji hao ni binti aliyetambulishwa kwa jina bandia la Anjela, ambaye anasema Mchungaji huyo alimdhalilisha kingono akiwa na umri wa maika 16 tu, alipoenda kanisani kwake kufanyiwa maombi kitendo kilichomfanya akose imani na makanisa yote duniani.
Anjela anasimulia alichofanyiwa na Alph Lukau
“Mwaka 2013 ulikuwa mwaka wenye maumivu sana kwangu, nililia usiku na mchana, nilikuwa najilaumu sana kwa kwenda katika lile kanisa. Ilinichukua miaka mitatu kuweza kuamini tena kanisa lingine tena”, alisema Anjela alipokuwa akihojiwa na chombo cha habari cha City Press cha Afrika Kusini.
“Baada ya miezi mitatu ya kutafuta kuonana na baba (Mch. Lukau), siku ikatimia, ilikuwa ni kutimiza ndoto. Alipofungua mdomo wake alizungumzia blauzi yangu na nywele zangu, aliniuliza kuhusu maisha yangu ya kimapenzi, ilinichanganya na kunifanya nisiwe sawa, na nilipomwambia kuwa bado ni bikira, alionekana kushindwa kuzuia furaha yake”, amesema Anjela
Anjela aliendelea....... “tulizungumza kwa zaidi ya saa moja, hatukugusia kitu chochote kuhusu biblia au maombi, baada ya hapo akaniambia nirudi siku nyingine, nilivyorudi alinitaka niwe mtu wa mwisho kuingia ofisini kwake kwani suala langu lilikuwa kubwa, hivyo nilivyoingia nilifurahi kwa kujua naenda kupata ukombozi, safari hii aliniangalia machoni akaniambia nataka nikusaidie, lakini ili mimi niweze kufanya hivyo unatakiwa urelax na uwe huru kwangu”.
"Alitaka tufanye ngono na kunishika kiunoni, na akaniambia tufanye mapenzi saa 6:00 mchana katika maeneo ya kanisa, na kuniambia safari nyingine nikikuona nataka uvue nguo. Kama hauko 'comfortable' hapa, tunaweza chukua chumba cha hoteli na tufanyie huko. Niliogopa na kutetemeka ingawa nilikuwa bado namuamini kwa sababu nikiamini ni mtumishi wa Mungu, akaniambia nipige magoti, na nikafanya kila alichoniambia”, amesimulia Anjela.
Anjela anasema hakuweza kumfungulia kesi kwa wakati huo kwa sababu aliamini hakuna atakayemuamini akimuelezea, kutokana na Alph Lukau kuwa mtumishi wa Mungu aliyekuwa akiminika sana, lakini aliishi akiumia moyoni bila kumwambia yeyote.
Anjela anasema hata walipokuwa wakikutana wafanyakazi wake walikuwa wakimuona kwani huwepo muda wote, hata mkewe kuna siku alimkuta ofisini kwake yuko naye anazungumza.
Hata hivyo Mchungaji huyo amekanusha madai hayo, na kusema kwamba yamepangwa ili kumchafua, kwani hawezi kufanya vitendo vya kumchukiza Mungu.
Habari zaidi kutoka City Press zinasema kwamba Anjela siyo mtu pekee kulalamika, kwani kuna mwanamke mwengine aliyewahi kuhojiwa naye alisema Mchungaji huyo alishawahi kumlazimisha kufanya mapenzi wakati akimuombea, na kumwambia asijali kwani Mungu atawasamehe.
Social Plugin