Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Charles Kuyeko (Chadema) leo Jumamosi Machi 23, 2019 ametangaza kujiuzulu uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.
Kuyeko ambaye ni diwani wa Bonyokwa amesema anamshukuru Rais wa Tanzania, John Magufuli Kwa kazi ya ajabu ya kutukuka ambayo anaifanya na kuomba Watanzania kumuunga mkono.
"Rais Magufuli ni mtu wa kuigwa, anastahili sifa na kazi ya kutukuka, nawaheshimu Viongozi wa CHADEMA kwa kunipa nafasi, nawashukuru na nitaendelea kuwaheshimu lakini mapenzi yangu ya dhati ni CCM" Amesema
Social Plugin