Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAITI SITA ZAOKOTWA ZIKIWA UCHI MBUGANI


Maiti zilivyookotwa
Miili sita ya watu wa jinsia ya kiume, imeokotwa katika mbuga ya wanyama ya Tsavo nchini Kenya, huku ikiwa utupu.

Miili hiyo imegunduliwa na maafisa wanyama pori wa hifadhi hiyo, ambao walikuwa kwenye patrol mbugani, ambapo walihisi harufu kali na kuamua kuanza kuchunguza, na ndipo walipokuta miili hiyo.

Polisi nchini Kenya imesema kwamba miili hiyo imepelekwa katika hospitali ya Makindu kwa ajili ya uchunguzi zaidi juu ya vifo vyao.

Hata hivyo jeshi la polisi linaamini kwamba watu hao hajafia katika mbuga hiyo, isipokuwa huenda waliuawa sehemu nyingine na kwenda kutupwa hapo.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com