Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo na watu wengine watatu wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata ajali na kupinduka.
Tukio limetokea eneo la Mandawa jana saa mbili usiku wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi wakati mkuu huyo akiwa safarini kwenda Dar es Salaam.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine, Muhaji Mohamedi amesema amepokea majeruhi wanne ambao ni Aziza Mangosongo, Mwanahamisi Naenda, mkazi wa Kitangali, Zaituni Lipau na Jasiri Nguru.
Amesema wanatarajia kuwapa rufaa majeruhi kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatus Chalya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema dereva Daudi Kakulilo wa gari hilo la Serikali anashikiriwa na polisi kwa mahojiano.
Social Plugin