Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATU 157 WAHOFIWA KUFA BAADA YA NDEGE KUANGUKA IKIELEKEA NAIROBI



Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.

Inaelezwa kuwa watu 157 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya ndege kuanguka leo.

Taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo zilifahamika dakika sita baada ya kuondoka kuelekea Nairobi, asubuhi ya leo saa mbili na robo na kuanza kupoteza mwelekeo ikiwa angani.

Ndege hiyo ilikuwa na abiria 149 na wafanyakazi wanane wa shirika la ndege nchini humo waliokuwa kwenye safari ya kuelekea Nairobi.
Ofisi ya waziri Mkuu wa Ethiopia Abey Ahmed imetoa taarifa ikitoa rambi rambi kwa familia za walio wapoteza wapendwa wao katika jali hiyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com