Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA UTENDAJI KAZI WA TAKUKURU......ASIMULIA ALIVYOAGIZA MAKADA WA CCM WAKAMATWE


Kamishna wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Diwani Athmani amesema taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh70.3 bilioni ikilinganishwa na Sh14.6 zilizookolewa mwaka 2016/2017.

Mbali na fedha hizo, amesema taasisi hiyo pia imefungua kesi 495 za rushwa katika kipindi cha mwaka 2017/2018 ikilinganishwa na kesi 435 zilizofunguliwa mahakamani mwaka 2016/2017.

Kamishna Athmani amesema hayo wakati akiwasilisha kwa Rais John Magufuli ripoti ya utendaji kazi wa Takukuru leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baada ya taarifa hiyo,  Rais  Magufuli amesisitiza umuhimu wa   wananchi kuendelea  kupiga vita suala la rushwa kwa lengo la kukuza maendeleo ya nchi huku akiwataka wafanyakazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutumia chombo hicho vizuri na kufanya utafiti wa haki usio wa kuwaonea watu bali kuwatendea haki.

“Rushwa ni ugonjwa kuliko hata saratani na ndiyo maana ninawaomba Watanzania kwa ujumla tupambane na rushwa na ninapongeza juhudi ambazo zinaendelea kufanywa na pongezi za kimataifa tunazozipata kutokana na kupambana na rushwa.

“Siku nne zilizopita nilipigiwa simu na raia flani kuwa Viongozi wa CCM wanataka rushwa pale Ilala, nikasema washikwe wakiwa na nguo za kijani, Rushwa haina chama, ukimkuta CCM kamata, ukimkuta CHADEMA kamata na hata wasio na chama.

"Sasa kwa vile wewe ni mtumishi wa TISS, mtu wa TISS akifanya makosa pia mkamate, pia msaidizi wako ni Mwanajeshi Brigedia Jenerali akila rushwa Mwanajeshi pia mnamkamata " Amesema Rais Magufuli



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com