Mamia ya wananchi wamefurika Uwanja wa Ndege Bukoba kushiriki mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Tanzania na aliyekuwa mhamasishaji mkubwa wa vijana katika matumizi ya vipaji na fursa, Ruge Mutahaba.
Magari mawili yatakayoongoza msafara tayari yameingia ndani huku 'plate number' zikiwa na maandishi ya R.I.P Ruge.
Pia magari yatakayohusika katika msafara yamepewa namba na kuandikwa neno 'msiba,na njiani kuna vibao vinavyoelekeza eneo la msiba kwenda Kijiji cha Kiziru Wilaya ya Bukoba.
Ndege ya ATCL iliyotua uwanjani hapo na baadaye kuondoka ilikuwa na abiria ambao wengi wao hawakuondoka na badala yake kujiunga na watu waliopo kiwanjani.
Baada ya mapokezi msafara utapita mitaa mbalimbali kuelekea Kiziru ambapo ataagwa kesho Jumatatu asubuhi viwanja vya Ghmkhana na mazishi kufanyika baadaye jioni.
Social Plugin