Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Helene Weesie (katikati), Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT) Mary Rusimbi (kushoto) na Mwenyekiti wa wanawake wa SBL, Anita Rwehumbiza wakiwa wameshika jumbe mbalimbali zilizotolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani (IWD) yaliyofanyika siku ya Ijumaa (Machi 15, 2019) katika Ofisi za Kampuni hiyo Masaki jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Aneth Harrison Afisa Ugavi, Naike Shile (katikati) na Annamary Laurean wakiwa na mabango yenye kuonyesha jumbe mbalimbali kuhusu maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani (IWD) ambapo kampuni hiyo imeadhimisha siku hiyo kwa kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii na taasisi.
Wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti kutoka kiwanda cha Moshi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani (IWD) yaliyofanyika katika Hoteli ya Keys ambapo kampuni hiyo imeadhimisha kwa kutambua umuhimu wa mwanamke katika maendeleo ya taasisi na jamiii.
Wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti kutoka kiwanda kilichopo mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani (IWD) ambapo kampuni hiyo imeadhimisha kwa kutambua umuhimu wa mwanamke katika maendeleo ya taasisi na jamii.
Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Zuwena Mohammed maarufu kama ‘Shilole’ akitumbuiza pamoja na wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani (IWD) ambapo kampuni hiyo imeadhimisha kwa kutambua umuhimu wa mwanamke katika maendeleo ya jamii na taasisi.
***
Dar es Salaam, Ijumaa Machi 15, 2019. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) jana waliungana kwa pamoja kuadhimisha siku hiyo huku wakihimizwa kujiamini sehemu za kazi.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie,Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT), Mary Rusimbi pamoja na wafanyakazi kutoka idara mbalimbali.
Mbali na Dar es Salaam maadhimisho hayo pia yalifanyika katika viwanda vilivyopo Mwanza na Moshi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie alisema kampuni hiyo imekuwa ikiweka mkazo katika kuwainua wanawake katika nafasi mbalimbali ili kufikia usawa wa kijinsia kwakuwa mwanamke ana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo katika jamiii na taasisi.
Usawa wa kijinsia umehimizwa katika maadhimisho yam waka huu kupitia kauli mbiu isemayo “Badili Fikra kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”.
“Wanawake wamekuwa msingi mkubwa katika nyanja za ufanyaji maamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi maeneo ya kazi hivyo kuna haja ya kutoa nafasi kwa wanawake wengi zaidi kwenye taasisi zetu ili kufikia usawa wa kijinsia na zaidi kufikia maendeeleo endelevu,” alisema Weesie.
Hata hivyo, aliwataka wanawake kujiamini zaidi ili waweze kupata nafasi za juu huku akihimiza kutosita kuonyesha ujuzi walionao kwani ndiyo msingi wa mafanikio.
Naye, Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT) Mary Rusimbi alisema wanawake wameendelea kushiriki kwa kasi katika ngazi za uongozi katika jamii na taasisi na kwamba hiyo ni ishara nzuri katika kuufikia usawa wa kijinsia hapa nchini.
Aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake na kuwapa jukwaa maalumu la wanawake liitwalo ‘SBL Spirited women’ ili kutoa nafasi ya kuboresha utendaji wao.
“Wanawake ni viongozi sio tu katika kuongeza tija lakini ni viongozi katika kushika shirika likae pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi wanazozifanya endapo ujuzi wao utatumika vizuri,” alisema Rusimbi.
Social Plugin