Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa haya : MCHUNGAJI ABATIZA WAUMINI KWA 'SODA BARIDI'...TAZAMA HAPA


Mchungaji akibatiza kwa soda
Huku visa vingi vikiibuka kuhusu mbinu mbalimbali wanazotumia wachungaji kuwavutia waumini katika makanisa yao wakidai ni miujuzi, mchungaji mwingine amejitokeza na kutangaza mbinu yake mpya. 

Katika video inayosambaa  ya mtandaoni  mchungaji huyo amewaacha wengi na mshangao mkubwa kwa mbinu yake ya kuwatakasa wenye dhambi na kuwaingiza katika Ukristu.

 Katika video hiyo, mchungaji alionekana akitumia soda kuwabatiza waumini wake badala ya maji safi ya mtoni ama ya chupa.

 Huku amesimama eneo la juu kiasi, mchungaji huyo alikuwa na chupa ya soda mkononi akiwamiminia waumini wake kinywaji hicho vichwani. 

 Waumini wanaonekana katika video hiyo wakiwa kwenye foleni kila mtu akisubiri kumiminiwa soda 'takatifu'.

TAZAMA VIDEO HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com