Pichani ni Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahamashisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Jumapili Machi 24, kuishangilia Taifa Stars katika mchezo wake dhidi ya Timu ya taifa ya Uganda.
Matokeo ya ushindi dhidi ya Uganda yanaweza kuipa Stars nafasi ya kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwezi Juni nchini Misri.
Hata hivyo ili Stars iweze kufuzu lazima Cape Verde iifunge au itoke sare na Lesotho. Mchezo baina ya timu hizo utapigwa huko Cape Verde muda sawa na mchezo kati ya Stars dhidi ya Uganda utakaopigwa kesho saa 12 jioni
Wapinzani wa Stars, Uganda Cranes wanatarajiwa kuwasili nchini leo. Uganda iliweka kambi ya wiki moja nchini Misri kujiandaa na mchezo huo
Social Plugin