AI, TEKNOLOJIA MPYA KATIKA SIMU NCHINI.
Baada ya uzinduzi rasmi wa Infinix ZERO 6 nchini Tanzania, simu yenye teknolojia ya Artificial intelligent, wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na ufanyaji kazi wa teknolojia hiyo, hivyo basi leo ningependa kuwajuza namna teknolojia ya AI kwenye kamera za Infinix ZERO 6 inavyofanya kazi.
Pamoja na sifa zingine nzuri za infinix ZERO 6, sifa kuu zaidi ya Infinix ZERO 6 ni kamera , Infinix Zero 6 imewekwa nguvu nyingi sana upande wa kamera ambapo kamera za nyuma ni MP 12+MP 24 zenye kupiga picha/picha jongefu na mng’ao wa hali ya juu sana, na kamera ya mbele ni MP 20.
Na katika kuongeza ubora wa kamera ya Infinix ZERO 6, ndipo teknolojia ya AI inapofanya kazi sambamba na kamera. Teknolojia ya AI inaiwezesha ZERO 6 kupiga picha zenye muonekano halisi ya mazingira husika mfano kama ni bahari au ua basi utapata picha zenye rangi halisi ya vitu hivyo.
Vile vile kioo cha mbele kimewekewa ulinzi kioo cha Gorilla inchi 6.2. Uwezo wake wa betri ni 3650mAh pamoja na XCharge kwa ajili ya teknolojia ya kuchaji haraka
Mbali na kamera, imekuwa ni kama tamaduni kwa Infinix kuzalisha simu zenye muoneka wa kuvutia na safari hii tunawapa asilimia 100% kwani wamehama kabisa kutoka material ya plastic na metal hadi kwenye alminium na class.
Infinix imezingatia swala la rangi, Infinix Zero 6 imekuja na rangi tatu tofauti Milan Black, Sapphire Cyan na champagne gold, simu hii inatikana nchi nzima .
sifa za zero 6.
Infinix ZERO 6 Specifications:
|
Network: 4G/3G/2G
|
OS Version: AndroidTM 8.1
|
Display: 6.18 INCH FHD+
|
Processor: Qualcomm SDM 636
|
Dimensions: 156.8*75.9*7.95mm
|
ROM + RAM: 64GB + 6GB
|
Battery: 3650mAh
|
Front camera: 12MP AF+24MP AF WITH QUAD FLASHLIGHT
|
Back camera: 20MP 4IN1 WITH FLASHLIGHT
|