Picha : TVMC YAENDESHA MAFUNZO YA KUTENGENEZA BATIKI KWA VIKUNDI VYA WAZAZI ....WAZINDUA BATIKI MATATA


Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC) Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO limeendesha mafunzo ye kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi vinavyojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto na ujasiriamali kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.



Mafunzo hayo ya siku nne yalianza Machi 21 na kumalizika Machi 25,2019 katika ukumbi wa SIDO mkoa wa Shinyanga kwa kukutanisha washiriki 25 yakiwa na lengo la kuwakwamua kiuchumi,kuondokana na umaskini ili kuzuia mimba na ndoa za utotoni sambamba na kuanzisha viwanda vidogo vidogo.


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia alilipongeza shirika la TVMC kumsaidia Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kutengeneza viwanda.

“TVMC mmeonesha kwa vitendo kuwa mnaunga mkono serikali ya Viwanda,tunawapongeza kwa kufanya kazi nzuri inayofuata matakwa ya serikali,tunaamini kuwa kupitia mafunzo haya,tutapata viwanda vidogo kutoka wajasiamali hawa na tunafurahi mmetoa mafunzo kwa kushirikiana na SIDO”,alieleza Mbia.

Aidha alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwainua kiuchumi wananchi huku akiwataka wajasiriamali kuomba mikopo kwenye halmashauri za wilaya ili kuendeleza shughuli zao.

Kwa Upande wake,Mkurugenzi wa Shirika la TVMC, Musa Ngangala alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni unaotekelezwa na TVMC kwa ufadhili wa shirika la Firelight Foundation la nchini Marekani.

“Ili kufanikisha mradi huu,mwaka 2016 tulianzisha vikundi vya ujasiriamali kwa wazazi ili kuhakikisha tunawakwamua kiuchumi ili kuondokana na umaskini ambao huchangia kwa kiasi kikubwa mimba na ndoa za utotoni,na kwa muda wa siku nne tumetoa mafunzo ya kutengeneza batiki”,alieleza Ngangala.

“Ili kuunga mkono kwa vitendo sera ya serikali ya Viwanda kupitia kwa Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli,Tunatarajia kuanzisha vyumba maalum kwa ajili ya shughuli ya utengenezaji batiki na tutatoa vitendea kazi vya kuanzia ili kuhakikisha vikundi hivi vinakuwa vya mfano katika Manispaa ya Shinyanga lakini mkoa kwa ujumla”,alisema Ngangala.

Hata hivyo Ngangala alisema TVMC itaendelea kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ili kuwapa ujuzi wananchi wafanye shughuli za ujasiriamali ili kuwaletea maendeleo.

Mara baada ya mafunzo ya Utengenezaji Batiki kumalizika,umefanyika uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.

Angalia Matukio katika picha hapa chini
Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi vinavyojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto na ujasiriamali kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga yaliyoendeshwa na SIDO kwa ufadhili wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness Elia,kulia ni Mkurugenzi wa TVMC,Musa Ngangala. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Musa Ngangala akielezea lengo la kutoa mafunzo ya utengenezaji batiki kwa vikundi vya wazazi vinavyojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto na ujasiriamali katika kata ya Chamaguha.

Mkurugenzi wa TVMC ,Musa Ngangala akiishukuru serikali kwa kuendelea kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.

Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza batiki kwa vikundi vya wazazi vinavyojihusisha na masuala ya ulinzi na usalama wa mtoto na ujasiriamali kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga.


Washiriki wa mafunzo ya utengenezaji batiki wakiwa ukumbini.
Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness  na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakiwa wameshikilia batiki iliyotengenezwa na vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha wakati wa uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Kulia ni Mkurugenzi wa TVMC ,Musa Ngangala akifurahia batiki ya ukweli.
Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC ukiendelea.
Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Pichani ni miongoni mwa batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka Chamaguha.
Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC ukiendelea.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la PACESH, Perpetua Magoke aliyealikwa kushuhudia kazi ya wajasiriamali wa Chamaguha.
Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Manispaa ya Shinyanga,Salome Komba akizungumza wakati kufunga mafunzo ya utengenezaji batiki.Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Chamaguha,Fatuma Msusa,kushoto ni Mkurugenzi wa TVMC ,Musa Ngangala.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga,Octavina Kiwone akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya utengenezaji batiki.
Zoezi la utoaji vyeti kushiriki na kufuzu mafunzo ya utengenezaji batiki likiendelea.
Utoaji vyeti ukiendelea.
Zoezi la kutoa vyeti kwa washiriki wa mafunzo likiendelea.
Utoaji vyeti ukiendelea.

Mshiriki wa mafunzo hayo,Gladness Mwita akitoa neno la shukrani kwa kupatiwa mafunzo ya kutengeneza batiki.
Mshiriki wa mafunzo hayo,Ramadhan Hamis akielezea kuhusu vikundi vya ujasiriamali vilivyoanzishwa na TVMC.


Awali washiriki wa mafunzo ya utengenezaji batiki wakitengeza batiki kwa kutumia mishumaa.


Utengenezaji batiki kwa vitendo ukiendelea.

Washiriki wa mafunzo hayo wakitengeneza batiki.
Utengenezaji batiki ukiendelea.
Zoezi la kuchanganya rangi likiendelea.
Batiki ikitolewa kwenye rangi.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ya utengenezaji batiki.

Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post