Mwanamke mmoja nchini China amegundulika kuwa na ugonjwa wa ajabu, ambao huripotiwa mara chache sana kwa watu.
Mwanamke huyo ambaye amejulikana kwa jina la Chen, aliamka na kujikuta hawezi kusikia sauti ya mpenzi wake, na kuamua kwenda Hospitali.
Alipofanyiwa vipimo na madaktari, mwanamke huyo aligundulika kuwa na tatizo hilo, ambapo yeye husikia sauti zote kasoro za wanaume tu pekee.
Tatizo hilo linajulikana kwa jina la 'reverse-slope hearing loss', ambao humfanya mtu kusikia sauti zenye 'mawimbi mazito' pekee. Ugonjwa huo hutokea nadra sana, ambapo imetajwa kuwa kati ya watu 13,000, mtu mmoja tu ndiye anayeweza kuwa na hatari ya kukubwa na ugonjwa huo.
Ugonjwa huo unaweza kusababishwa na vinasaba ambapo pia mtu anaweza akawa hajawahi kusikia sauti ya chini mfano ile ya muungurumo wa friji, na asigundue tofauti.
Kwenye kesi ya bi Chen, imegundulika kuwa alikuwa akifanya kazi kupitiliza, na kuufanya mwili wake kuchoka, kukosa usingizi na kumfanya apate msongo wa mawazo uliompeleka kupata tatizo hilo la kusikia sauti za wanawake pekee.
Social Plugin