Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UVCCM YATANGAZA KUMSAMEHE LOWASSA


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kupitia Mwenyekiti wake Kheri James umesema kwa sasa umemsamehe Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa baada ya kutangaza kurejea chama hicho.

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema umoja huo umeona hauna budi kuanza kurasa mpya na Waziri Mkuu huyo wa zamani na kutaka watu ambao wanaamini Lowassa ni mkosefu wajitokeze.

Kheri James amesema, "amekiri na anaanza upya na ndiyo maana hakurudishiwa uanachama wake wa zamani bali ameenda katika tawi lake na kuomba upya uanachama wa CCM.”

“Kila anayetaka kuwa mwanachama anatakiwa kufuata utaratibu kama wanachama wengine wanavyofanya," amesema Kheri.

Marchi 1, 2019, Edward Lowassa alitangaza kurudi ndani ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kukaa nje ya chama hicho kwa zaidi ya siku 1312.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com