Viongozi wa tatu wa Chama Cha Mapinduzi wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na kosa la kuomba milioni tano za rushwa kwa mwananchi aliyekuwa akitaka kupanga katika viwanja vya CCM.
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Christopher Myava, amesema kwamba Takukuru Ilala ilipokea taarifa Machi 22, kutoka kwa raia huyo aliyeombwa rushwa.
Viongozi hao wametajwa kuwa ni Jenipha Mushi Katibu wa CCM tawi la Amana, Ilala, Katibu Kata ilala, na Frank Mang'ati ambaye ni Katibu wa Hamasa Dar es salaam.
Amesema kwamba walitengeneza mtego baada ya kupewa taarifa ambapo mshtakiwa wa kwanza alikamatwa eneo la Msimbazi Sekondari akiwa na kiasi ch sh.milioni tatu huku wenzake wakiwa wanamsubiri katika eneo la klabu ya wazee kwa ajili ya mgao wa pesa.
"Miradi mingi ya CCM ambayo baadhi ya wanachama wasiokuwa waaminifu, wamekuwa wakiitumia vibaya, sasa nitoe wito kwao kwamba TAKUKURU haitosita kuwachukulia hatua za kisheria" - amesema Christopher Myava.
Ameongeza kwamba mapambano ya kupambana na rushwa yanatengemea sana taaarifa za wananchi hivyo wananchi wasiwe kimya wanapokutana na changamoto ya kushawishiwa kutoa taarifa.
Social Plugin