Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) mkoa wa Shinyanga (UVCCM) kwa kushirikiana na Taasisi ya Marafiki wa Dkt. Tulia Ackson 'Friends of Tulia' wameendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake lengo likiwa ni kutoa fursa kwao ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mafunzo hayo yanayotolewa pia na wakufunzi kutoka taasisi ya Mjasiriamali Kwanza Enterprises yamezinduliwa leo Machi 5,2019 kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ushetu wilayani Kahama.
Awali akizungumza,Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Barack Shemahonge, alisema katika kuelekea Tanzania ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati ni lazima wananchi wajitume kufanya kazi, jambo ambalo limemgusa na kuamua kuendesha mafunzo hayo ili kukuza uchumi wa kaya na taifa kwa ujumla.
Alisema moja ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuondoa umaskini kwa wananchi, hivyo kupitia mafunzo hayo ya ujasiriamali ambayo yanatolewa bure, ana imani kuwa maisha ya watu hao ambao wamejitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo yatabadilika na kukuza vipato kwenye kaya zao.
“Naomba pia mjiunge kwenye vikundi ili muweze kupata mikopo kwenye halmashauri asilimia 10, ili mpate mitaji na kupanua wigo wa biashara zenu na kuinuka kiuchumi ikiwa fedha ni za makusanyo ya mapato ya ndani na mikopo yake haina riba,”amesema Shemahonge.
Akizindua mafunzo hayo ya ujasiriamali, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wabunifu kwenye biashara zao pamoja na kuzingatia ubora wa bidhaa jambo ambalo litawafanya kupata wateja wengi na kukua kiuchumi.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu (CCM) mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga, aliwataka wajasiriamali hao kutokata tamaa pale wanapokumbana na changamoto katika biashara zao, bali wawe majasiri na kuendelea kupambana, kitendo ambacho kitawakomaza na hatimaye kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Nao baadhi ya wajasiriamali hao akiwemo Custa Mwambuli ambao wanafanya shughuli ya kutengeneza mkaa kwa kutumia karatasi, walipongeza utolewaji wa mafunzo hayo na kubainisha kuwa yatawapatia mbinu mbalimbali namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kutambulika kimataifa na hatimaye kukua kiuchumi.
Miongoni mwa mafunzo yanayotolewa kwenye semina hiyo ya ujasiriamali ni utengenezaji keki za harusi, mikate, sambusa,burger, ubuyu wa rangi, ufugaji wa kuku, nyuki, samaki, kilimo cha uyoga, sabuni za miche, dawa za usafi, mishumaa, karanga za mayai chaki za mashuleni, mafuta ya mgando, ushonaji wa mawigi, pamoja na mapambo ya sherehe.
Mafunzo hayo yatadumu kwa siku tatu kuanzia leo Machi 5,2019.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza kwenye uzinduzi wa semina ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo yatadumu kwa muda wa siku tatu kwa vijana na wanawake kupewa ujuzi na mbinu namna ya kuendesha biashara na kukua kiuchumi. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ushetu wilayani Kahama akizindua mafunzo ya ujasiriamali mkoani Shinyanga na kuwataka washiriki wawe wabunifu kwenye biashara zao pamoja na kuzingatia ubora wa bidhaa ili wapate wateja wengi na kukua kiuchumi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Haula Kachambwa akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali na kuwataka wayatumie vizuri katika kubadilisha hali ya maisha yao kiuchumi.
Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya Shinyanga Mjini wakiwa kwenye uzinduzi wa mafunzo yao ya kutengeneza bidhaa mbalimbali pamoja na kupewa mbinu za kibiashara ili wapate kukua kiuchumi.
Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya Shinyanga mjini wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi mbalimbali juu yao kabla ya kuanza kufundishwa namna ya kutengeneza bidhaa na mbinu za kibiashara.
Wajasiriamali wakiendelea kusikiliza nasaha za viongozi kabla ya kuanza kufundishwa namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Marafiki wa Dkt. Tulia Ackson mkoani Shinyanga Shabani Wisandara akitambulisha marafiki wa taasisi hiyo ambayo imejipanga katika kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuhudumia wananchi.
Usikilizaji wa nasaha ukiendelea kabla ya kuanza ufundishwaji wa kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Msemaji wa Taasisi ya Dkt Tulia Ackson nchini Tanzania Matiko Nyaiho akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wameshirikiana na UVCCM mkoa wa Shinyanga, kuleta mafunzo hayo ya ujasiriamali bure kwa vijana na wanawake ili kuwafundisha namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali na hatimaye kujikwamua kiuchumi.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) kwa kuleta mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake mkoani humo, ili kuwakwamua kiuchumi.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akimpatia cheti cha pongezi Mwenyekiti wa taasisi ya Marafiki wa Dkt. Tulia Ackson kwa kushirikiana na UVCCM Mkoa wa Shinyanga kuleta mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na wanawake ili kuwa kwamua kiuchumi na katika kuelekea Serikali ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa naye akionyesha cheti cha Pongezi katika kushirikia kuzindua mafunzo ya ujasiriamali na kutoa mbinu za namna ya kufanikiwa kibiashara.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akikagua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali ambao walifika kwenye mafunzo hayo kuongeza mbinu namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kukua kiuchumi.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa, akiwasisitiza wajasiriamali kuyatumia vizuri mafunzo hayo kujikwamua kiuchumi.
Custa Mwambuli ni mjasiriamali ambaye anafanya shughuli ya kutengeneza mkaa kwa kutumia karatasi, akipongeza utolewaji wa mafunzo hayo kuwa yatawapatia mbinu mbalimbali namna ya kupanua wigo wa biashara zao na kutambulika kimataifa na hatimaye kukua kiuchumi.
Awali Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa (kulia) akijiandaa na hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya ujasiriamali, katikati ni mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, na kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Dotto Joshua.
Mbunge wa Viti Maalumu Lucy Mayenga (kushoto) akiwa na msemaji wa Taasisi ya Friends of Dkt Tulia Ackson, Matiko Nyaiho mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa mafunzo ya ujasiriamali.
Awali Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Elias Kwandikwa akiwasili ukumbini kwenda kuzindua mafunzo ya ujasiriamali kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, akiwa na mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Baraka Shemahonge.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akipiga picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM.
Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Social Plugin