Katibu Tawala DAS Ilala Sheila Edward aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akitoa neno wakati wa sherehe ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Tanki la Maji katika eneo la Majohe jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Ilala Upendo Lugongo akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza na wananchi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Diwani wa Mtaa Kichangani Mwenevyale Waziri akitoa neno.
Wakazi wa Majohe na vitongoji vyake wakisikiliza kwa makini.
Katibu Tawala DAS Ilala Sheila Edward akiwa sambamba na Diwani wa Mtaa Kichangani Mwanevyale Waziri wakiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita 150,000 litakalohudumia wananchi laki saba (700,000) leo Jijini Dar es Salaam.
Shamra Shamra zilitanda.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wakazi zaidi ya 700,000 wa Majohe na vitongoji vyake jijini Dar es Salaam wanatarajia kupatiwa majiSafi na Salama ifikapo mwishoni mwa mwezi Aprili 2019.
Serikali kuwajengea Tanki la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi Lita 150,000 kwa siku katika Mtaa wa Kichangani.
Akiweka jiwe la Msingi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Katibu Tawala DAS Sheila Edward amesema kuwa mradi huu utawasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kuwapunguzia kero ya maji waliyonayo kwa muda mrefu.
Amesema, serikai inaendelea kutekeleza ahadi za serikali ya mapinduzi ili kufikia malengo ya kumtua mama ndoo kichwani na wamekuwa wanashirikiana na madiwani kwani maendeleo hayana chama.
DAS amesema, Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa maji Mtaa wa Kichangani Majohe utasaidia wananchi takribani laki saba (700,000) kuondokana na kero na amezitaka mamlaka husika kusimamia mradi huo pindi utakapomalizika ili uweze kujiendeleza.
Kaimu Mkurugenzi Wa Manispaa ya Ilala Mhandisi Upendo Lugongo amesema kuwa mradi huo wa maji unajengwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA na utawasaidia wananchi wote wanaoishi mtaa wa Kichangani Mahoje.
Amesema kuwa, gharama za mradi huo ni takribani milioni 230 na unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa nne na lengo kuu ni kupunguza kero ya maji kwa wananchi.
Upendo amesema, serikali kwa kushirikiana na mamlaka za maji wanaendelea kushirikiana kwa pamoja kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayakuwa na mtandao wa maji na kufikia lengo la asilimia 95 mwaka 2020.
“Kuna mradi mwingine wa maji unaosimamiwa na DAWASA wa Ujenzi wa tanki la Kisarawe ambapo kufikia mwishoni mwa mwaka huu wananchi wote wa Majohe na Gongo la Mboto kwa ujumla watapata majisafi na salama,” amesema Upendo.
Diwani wa Kata ya Kichangani Mwenevyale Waziri ameishukuru ofisi ya Mkurugenzi kwa kufanikisha kuja kwa mradi huo kwani wana muda mrefu wananchi wa eneo hilo hawajapata majisafi na salama.
Mradi huo wa maji wa Mtaa wa Kichangani utakapomalizika kutajengwa vizima saba vya kuchotea maji kwa ajili ya kuwarahishia wananchi wa maeneo hayo.
DAWASA wanaendelea kuadhimisha wiki ya maji iliyoanza Machi 16 na itamalizika Machi 22 ikiwa na kauli mbiu ya Hakuna atakayeachwa.
Social Plugin